Tovuti mpya inaleta habari kuhusu Coronavirus katika lugha 25

Tovuti mpya inaleta habari kuhusu Coronavirus katika lugha 25

Kupitia tovuti hii na simu hotline unaweza kupata majibu ya maswali yako kuhusu coronavirus katika lugha yako mwenyewe. Hotline yetu na huduma ya mazungumzo ni ya wafanyakazi na wataalamu wa lugha wenye kutumika na hizo lugha 25. Kati ya 14 jioni hadi saa 16 jioni kila siku unaweza kuongea au kuandikiana na mfanyakazi kwa lugha yako mwenyewe. Wafanyikazi wana habari mpya kutoka Bodi ya Kitaifa ya Afya kuhusu coronavirus huko Denmark na wanaweza kujibu maswali mengi.

Hii wakati ikipita kati ya saa 14 jioni hadi saa 16 jioni, unaweza kuacha ujumbe kwenye huduma ya mazungumzo. Mfanyakazi wetu moja atakuletea jibu, siku ifwatayo kati ya saa 14.00 na 16.00. Tovuti pia italeta habari iliyochaguliwa na miongozo muhimu kutoka kwa mamlaka ya inchi.

Ni shirika la Denmark la Msada kwa Wakimbizi pamoja na shirika la ”Als Research” wanasimamia tovuti hii. Kazi hii inafadhiliwa na “Novo Nordisk Foundation”. Tunafanya kazi na mamlaka kuu ya Denmark kwa kuhakikisha kuwa maarifa yaliyowasilishwa hapa ni sahihi na hadi sasa.