Mpango wa kufungua tena Denmark iko mahali

Mpango wa kufungua tena Denmark iko mahali

Serikali imewasilisha mpango wa awamu ya 2 ya kufungua tena Denmark. Awamu ya 2 inajumuisha kufungua tena idadi ya maeneo ya kazi ya kibinafsi na ya umma. Kufungua upya ni kwa masharti juu ya shughuli zinaweza fanyikwa kwa njia nzuri ya kiafya na kuweka maambukizi chini ya udhibiti. Miongozo  kuhusu umbali wa mwili na wa usafi lazima viendelee kudumishwa.

Tupigie simu moja kwa moja kwa nambari yetu ikiwa hauna uhakika kufungua tena kwa Denmark inaamanisha nini kwako na familia yako.

 • Ufunguzi kamili wa biashara rejareja – maduka na maduka makubwa (Tarehe 11 Mei 2020)
 • Watoto wa darasa la 6 hadi 10 wanaweza kwenda shule tena (kuanzia tarehe 18 Mei 2020). Shule na manispaa wanakubaliana katika eneo lao jinsi ya kufungua tena itaweza fanyika ndani ya miongozo ya utunzaji wa afya.
 • Kufundisha na mitihani na mahitaji ya mahudhurio ya kimwili (Tarehe 18 Mei 2020) Ufunguzi wa STU, EUD na R&D (Tarehe 18 Mei 2020)
 • Mikahawa na maduka kama haya zinaweza kutumika (kuanzia tarehe 18 Mei 2020)
 • Makanisa ya Folkekirke na makanisa na dini zingine zafunguliwa (kuanzia tarehe 18 mei 2020)
 • Kufanya kazi nyumbani kwa ma kampuni za kibinafsi
 • Michezo za kitaalam zinaweza tendeka lakini ifanyike bila ya watazamaji
 • Kukopesha na kurudisha vitabu kwenye maktaba (kuanzia Tarehe 18 Mei 2020)
 • Michezo na mazoezi na vilabu vya nje vinafungua
 • Kumaliza kwa uendelezaji katika shule za sekondari (Tarehe 18 Mei 2020)
 • Nafasi ya maonesho ya wanyama ambazo wageni husafirisha wenyewe kwa gari zinaweza kuwa wazi

 

Serikali iko kwenye mazungumzo na nchi jirani na itaamua juu ya udhibiti wa mipaka wa muda wa marufuku ya kuingia na miongozo iliyoongezeka kuhusu safiri. Serikali itatangaza hii ifikapo tarehe 1 Juni 2020.